Assad aligeukia kundi la BRICS kumaliza vita Syria | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.03.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Assad aligeukia kundi la BRICS kumaliza vita Syria

Rais wa Syria, Bashar al Assad, amelitaka kundi la mataifa yanayoinukia kwa kasi kiuchumi, BRICS, kusaidia kumaliza machafuko nchini mwake na mateso yanayowakabili watu wake.

Syria's President Bashar al-Assad speaks at the Opera House in Damascus in this still image taken from video January 6, 2013. REUTERS/Syrian TV via Reuters TV (SYRIA - Tags: POLITICS PROFILE TPX IMAGES OF THE DAY) NO SALES. NO ARCHIVES. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. IT IS DISTRIBUTED, EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS. SYRIA OUT. NO COMMERCIAL OR EDITORIAL SALES IN SYRIA

Bashar al-Assad Rede TV Fernsehen Staats TV

Uamuzi wa Assad kuzigeukia nchi za BRICS unakuja wakati mkuu wa zamani wa tume ya uangalizi ya Umoja wa Mataifa nchini Syria akisema wakati umewadia kutafakari kutangaza marufuku ya ndege kuruka katika anga ya Syria.

Mwito wa rais Assad kwa kundi la mataifa ya BRICS, yakiwemo, Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, umekuja wakati shirika la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International likisema ulimwengu unatakiwa kuzishinikiza pande zote katika mzozo wa Syria, kukomesha uhalifu na uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

"Nawatolea mwito viongozi wa nchi za BRICS kushirikiana pamoja kukomesha mara moja machafuko nchini Syria ili kuhakikisha suluhisho la kisiasa linafaulu," alisema Assad kwenye barua aliyomuandikia rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma. "Hii inahitaji ari ya kimataifa iliyo wazi ili kuzikausha raslimali za magaidi na kusitisha ufadhili na silaha wanazopewa," aliendelea kusema Assad katika barua hiyo iliyochapishwa na shirika la habari la serikali, SANA.

Lakini Assad alisema mateso ya Wasyria yalisababishwa na vikwazo vya kiuchumi visivyo halali ambavyo ni kinyume na sheria za kimataifa na vinavyoyaathiri moja kwa moja maisha na mahitaji muhimu ya raia. "Syria inataka kushirikiana na nchi za BRICS kama chombo cha haki kinachotaka kuleta amani, usalama na ushirikiano miongoni mwa nchi, mbali kabisa na dola moja kuwa juu ya dola nyingine na manyanyaso yanayolazimishwa kwa watu wetu na mataifa kwa miongo kadhaa," alisema Assad.

Kufuatia mkutano uliofanyika Durban, Afrika Kusini, viongozi wa kundi la BRICS walielezea wasiwasi wao mkubwa kuhusu kuzorota kwa usalama na hali ya kibinaadamu nchini Syria. Kwa kutumia busara viongozi hao walipinga miito ya nchi za magharibi kumtaka rais Assad aondolewe madarakani.

epa03642465 Indian Prime Minister Manmohan Singh (L), Chinese President Xi Jinping (2-L), South African President Jacob Zuma (C), Brazilian President Dilma Rousseff (2-L), and Russian President Vladimir Putin (L) pose for a picture during the 5th BRICS summit in Durban, South Africa, 27 March 2013. The agenda of the BRICS summit is expected to aim at the ways of global economic recovery. EPA/ALEXEY DRUGINYN / RIA NOVOSTI / KREMLIN POOL MANDATORY CREDIT +++(c) dpa - Bildfunk+++

Viongozi wa nchi za BRICS

Marufuku ya ndege katika anga ya Syria

Wakati huo huo, kiongozi wa zamani wa tume ya waangalizi ya Umoja wa Mataifa aliyejaribu na kushindwa kupata makubaliano ya kusitisha mapigano katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, Jenerali Robert Mood kutoka Norway, amesema wakati umefika kuiwekea Syria marufuku ya ndege kutoruka katika anga yake. Kauli yake imekuja baada ya katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO, Anders Fogh Rasmussen, kufutilia mbali harakati ya kijeshi ya nchi za magharibi kuingilia kati nchini Syria na kutoa mwito wa kutafuta suluhisho la kisiasa kwa mzozo huo wa miaka miwili uliosababisha vifo vya watu takriban 70,000.

Jenerali Mood amesema anapinga wazo la kuwapa silaha waasi wa Syria akisema anaamini silaha hizo hazitasaidia kupunguza mateso yanayowakabili wanawake na watoto katika vitongoji vya mji mkuu Damascus na Aleppo na miji mingine ya nchi hiyo.

Magari yapelekewa kikosi cha milima ya Gholan

Kwa upande mwingine Umoja wa Mataifa umetuma magari zaidi yasiyoweza kutobolewa na risasi na magari ya kubebea wagonjwa kwa ajili ya tume yake katika milima ya Gholan kwa sababu ya kuenea kwa machafuko ya Syria. Tangazo hilo la vifaa zaidi kwa ajili ya tume inayosimamia mkataba wa usitishwaji mapigano baina ya Israel na Syria lililotolewa na msemaji wa umoja huo, Josephine Guerrero, wakati baraza la usalama likielezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kitisho dhidi ya wanajeshi wa kulinda amani kutokana na mzozo wa Syria.

Nchini Syria kwenyewe ndege za kivita zimezishambulia ngome mbili za waasi kaskazini mashariki mwa mji mkuu Damascus jana. Hujuma hizo zilifanywa wakati waasi walipoviteka vituo vitatu vya jeshi karibu na mpaka wa usitishwaji wa mapigano kati ya Syria na Israel.

Mwandishi: Josephat Charo/RTRE/AFPE

Mhariri: Daniel Gakuba

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com