1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoRwanda

Arsenal kusitisha mkataba wa ushirikiano na Rwanda

19 Novemba 2025

Uongozi wa timu ya Arsenal umetangaza Jumatano kuwa utasitisha mkataba wa ushirikiano na nchi ya Rwanda ifikapo mwishoni mwa msimu huu baada ya kuafikiana na bodi husika mjini Kigali.

https://p.dw.com/p/53tiU
Ushirikiano wa Rwanda na timu ya Arsenal "Visit Rwanda"
Mkataba huo wa ushirikiano unaohusisha timu ya Arsenal kuchapisha kwenye jezi na vifaa vingine maandishi ya " Visit Rwanda".Picha: Jacques Feeney/Offside/IMAGO

Mkataba huo wa ushirikiano unaohusisha timu ya Arsenal kuchapisha kwenye jezi na vifaa vingine maandishi ya " Visit Rwanda", ulisainiwa misimu minane iliyopita na umekuwa ukikosolewa kutokana na vita vinavyoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo Rwanda imekuwa ikitajwa kuhusika.

DRC inaishutumu Rwanda  kwa kuwapa silaha na kuwaunga mkono wanamgambo wa M23, ambao wamechukua udhibiti wa maeneo mengi ya mashariki mwa Kongo. Hata hivyo Rwanda  bado ina aina hii ya ushirikiano na miamba wa Ulaya kama Paris Saint-Germain, Bayern Munich na Atletico Madrid.