ANKARA: Waturuki wachagua bunge jipya | Habari za Ulimwengu | DW | 22.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA: Waturuki wachagua bunge jipya

Uchaguzi wa bunge umeshafunguliwa nchini Uturuki, safari hii ukiwa na umuhimu mkubwa sana.Vyama 14 na wagombea 700 wanaojitegemea,wanapigania viti 550 bungeni.Uturuki,iliamua kuitisha chaguzi hizo mapema katika juhudi ya kupunguza mivutano ya kisiasa.Mivutano hiyo ilizuka,baada ya Waziri Mkuu,Recep Tayyip Erdogan,kumteua waziri wa mambo ya nje Abdullah Gul,kugombea wadhifa wa urais, hatua iliyopingwa vikali na upande wa upinzani usiofungamanisha masuala ya kisiasa na dini. Uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni, unaonyesha kuwa chama cha Erdogan cha AK,chenye mizizi ya siasa kali za Kiislamu,huenda kikabakia madarakani,wakati Chama cha Jamhuri ya Umma cha upande wa upinzani kikichukua nafasi ya pili. Kiasi ya watu milioni 42 kutoka jumla ya wananchi wapatao milioni 73 wanahaki ya kupiga kura katika uchaguzi wa hii leo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com