Amnesty: Mashambulizi ya Israel nchini Lebanon yachunguzwe
9 Julai 2026
Amnesty ilichunguza mashambulizi matatu yaliyolenga nyumba za raia kati ya Machi 6 na 13, ambapo jumla ya raia 24 waliuawa, wakiwemo watoto 12.
Shirika hilo lenye makao yake makuu mjini London limeishutumu Israel kwa "kuangamiza familia” katika mashambulizi hayo na kutaka yahesabiwe kuwa "uhalifu wa kivita”.
Limesema "Kwa kuzingatia ushahidi uliokusanywa, lina msingi wa kuridhisha wa kuhitimisha kwamba katika kila moja ya mashambulizi hayo ya anga, vikosi vya Israel vilikiuka sheria za kimataifa za kibinadamu ikiwa ni pamoja na kushindwa kutofautisha kati ya raia na malengo ya kijeshi.
Amnesty ilipowasiliana na mamlaka za Israel zilisema sehemu ya mashambulizi hayo "yalifanywa dhidi ya malengo ya kijeshi ya Hezbollah”, ingawa mengine "yanaendelea kuchunguzwa”.