1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aliyefungwa jela pamoja na Nelson Mandela afariki dunia

Sekione Kitojo
22 Julai 2020

Mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika  kusini Andrew Mlangeni amefariki dunia Jumatano akiwa na umri wa miaka  95.. Mlangeni, alifungwa jela pamoja na Nelson Mandela mwaka1964.

https://p.dw.com/p/3fgab
Südafrika Johannesburg | Andrew Mlangeni, Anti-Apartheid-Aktivist
Picha: Getty Images/AFP/

Mwanaharakati  wa  kupinga  ubaguzi  wa  rangi  nchini Afrika  kusini  Andrew Mlangeni amefariki dunia Jumatano. Mlangeni, ambaye  alifungwa  jela  pamoja  na  Nelson Mandela  mwaka 1964 baada  ya  kesi  ya  uhaini, amefariki akiwa  na  umri  wa  miaka  95.

Mlangeni, ambaye  alitumikia  kifungo cha  miaka  26  jela na  alikuwa  mshitakiwa  wa  sita  wa  kesi  hiyo maarufu  ya uhaini  kufariki, alilazwa  hospitalini kufuatia  mtatizo ya kifua, ofisi  ya  rais  wa  Afrika  kusini imesema  katika taarifa.

Rais Cyril Ramaphosa, ambaye  alipambana  pamoja  na Mlangeni kuleta  usawa  na  kufikisha  mwisho  utawala  wa wazungu  wachache nchini  humo, amemueleza  kuwa  ni nguzo ya uongozi wa kimaadili  na kujali ubinadamu, ambae kifo  chake  kinafikisha  mwisho wa  kizazi cha historia na kuweka mustakabali wa nchi  hiyo  katika mikono ya wale  waliobaki.

Mlangeni  alizaliwa  mwaka  1925 na  alijiunga  na  tawi la vijana  wa  chama  cha  ANC mwaka  1951,na baadae alipelekwa  nje  ya  nchi  hiyo  kwa  mafunzo ya kijeshi.