1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini kukamilisha mkakati wa ukuaji hivi karibuni

Oumilkheir Hamidou
30 Septemba 2019

Rais Ramahosa ameahidi mkakati wa kuchochea ukuaji wa kiuchumi na marekebisho utakamilika wiki chache kutoka sasa. Mkakati huo unajumuisha pia mipango ya kuifanyia marekebisho makampuni ya umma.

https://p.dw.com/p/3QULQ
Südafrika Präsident Cyril Ramaphosa
Picha: Reuters/R. Bosch

Serikali ya Afrika Kusini itakamilisha mkakati wa ukuaji wa kiuchumi katika kipindi cha wiki chache zinazokuja, amesema hayo rais cyril Ramaphosa,katika wakati ambapo nchi hiyo imepania kuinua imani kuelekea uchumi unaodhihirika kupwaya na nafasi za kazi kupunguwa. Imani ya wawekezaji katika nchi hiyo iliyoendekea kiviwanda barani Afrika ina lega lega huku ukuaji wa kiouchcumi ukionyesha kudorora kutokana na ukosefu wa hali ya uwazi na maendeleo katika sera za mageuzi. Katika hotuba yake ya kila wiki kwa taifa inayojulikana kama "kutoka dawaati la Rais Ramaphosa amesema baada ya mwongo wa kupungua ukuaji wa kiuchumi na umaskini  mkubwa, watu wanasubiri kuona ishara za maendeleo. Rais Ramahosa ameahidi mkakati wa kuchochea ukuaji wa kiuchumi na marekebisho utakamilika wiki chache kutoka sasa. Anamaanisha mkakati unaojumuisha pia mipango ya kuifanyia marekebisho makampuni ya umma mfano wa lile la nishati la esakom na kuanzishwa fuko la kufgharuimia miundo mbinu.