1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoQatar

Qatar: Watu 400 walikufa kwenye miradi ya Kombe la Dunia

Iddi Ssessanga
30 Novemba 2022

Afisa wa juu wa kombe la dunia nchini Qatar amesema zaidi ya wafanyakazi 400 wa kigeni walikufa katika ajali za kazini nchini humo katika miaka ya kuelekea michuano hiyo.

https://p.dw.com/p/4KHne
Wie klimafreundlich ist die WM in Katar? - Stadium 974
Picha: MIS/IMAGO

Hassan Al-Thawadi, kiongozi wa kamati ya utekelezaji na maandalizi, ametoa idadi ya vifo 400 hadi 500 katika mahojiano na televisheni ya Uingereza, alipoulizwa ni wafanyakazi wangapi walikufa wakifanya kazi ya kombe la dunia.

Hata hivyo kamati ya maandalizi imesema jibu lake lilimaanisha takwimu za kitaifa kwa kipindi cha kuanzia 2014 hadi 2020 kwa vifo vyote vyote vinavyohusiana na kazi nchini Qatar, na vikihusisha sekta zote na watu wa mataifa yote. 

Qatar haijawahi kutoa takwimu hasa za idadi ya vifo vya wafanyakazi wa kigeni, ingawa imekanusha madai ya mashirika ya haki za binadamu kuwa maelfu wamekufa. Mamlaka zimesisitiza ni wafanyakazi 37 wamekufa kwenye miradi ya kombe la dunia, na watatu tu katika ajali zinazohusiana na kazi.

Wafanyakazi wa kigeni wanachangia milioni 2.5 kati ya wakaazi jumla milioni 2.9 wa Qatar na mazingira ya kazi nchini humo yamekosolewa vikali - hasa katika miradi mikubwa ya ujenzi iliolibadilisha taifa hilo dogo katika muongo uliyopita.

-