Adidas yazindua Krasava
11 Novemba 2016Jina lake, Krasava, linaeleza neno linalotumiwa na mashabiki wa michezo wa Kirusi kusifia mchezo wa kusisimua.
Mpira huo utatumiwa kwa mara ya kwanza Novemba 14 kwenye mchuano wa kirafiki kati ya wenyeji wa dimba la Kombe la Mashirikisho na Kombe la Dunia 2018 Urusi na Romania. Kombe la Mashirikisho litachezwa katika miji minne ya Urusi kati ya Juni 17 na Julai 2, 2017.
Huwaleta pamoja mabingwa wa mashirikisho sita wanachama wa FIFA, pamoja na mabingwa wa dunia Ujerumani na wenyeji Urusi. Ureno (Ulaya), Australia (Asia), Mexico (Amerika ya Kaskazini, ya kati na Karibean), Chile ( Amerika Kusini) na New Zealand (Oceania) zimefuzu, wakati bingwa wa Afrika anasubiriwa.
Adidas ni mfadhili wa muda mrefu wa FIFA na pia ilitengeneza mipira iliyotumika katika mashindano yaliyopita ya Mashirikisho, kama vile Cafusa (Brazil 2013, Kopanya (Afrika Kusini 2009) na Pelias (Ujerumani 2005).
Mwandishi: Bruce Amani
Mhariri: Yusuf Saumu