2 wauawa na bomu Algeria | Habari za Ulimwengu | DW | 29.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

2 wauawa na bomu Algeria

ALGIERS:

Bomu lililokuwa ndani ya gari limelipuka katika mji wa Thenia nchini Algeria.Mji huo unapatikana umbali wa kilomita 55 mashariki mwa mji mkuu wa Algiers.Hakuna habari za haraka za majeruhi.

Taarifa moja kutoka kwa alieshuhudia imesema kuwa shabaha ya shambulio hilo kilikuwa kituo cha polisi.Mlipuko huo umetokea takriban mwezi mmoja baada ya shambulio lingine la bomu kwa kituo cha polisi katika mji wa Naciria,kilomita 75 magharibi mwa Algiers.Polisi wanne waliuliwa na wengine 20 kujeruhiwa katika shambulio hilo lilotokea januari 2.Hakujatokea kundi linalodai kuhusika na shambulio la leo ingawa tawi la Al Qaida la sehemu za kaskazini mwa Afrika ndio limekuwa likidai kuhusika na mashambulio mengine.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com