1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky alalamikia kutopewa silaha na Magharibi

10 Aprili 2024

Rais Volodymr Zelensky wa Ukraine amelalamikia tena kukosekana kwa msaada wa silaha kutoka mataifa ya Magharibi kwenye vita vya nchi yake dhidi ya uvamizi wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4ebDX
Ukraine
Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky Picha: Ukrainian Presidency/abaca/picture alliance

Akizungumza na gazeti la Bild la hapa Ujerumani hapa Ujerumani hapo jana, Zelensky alisema licha ya washirika wao wa Magharibi kuwa na silaha wanazohitaji ili waweze kuishi, hafahamu kwa nini hawapewi silaha hizo.

Zelensky aliyasema hayo akiwa kwenye mkoa wa Kharkiv, mashariki mwa Ukraine, ambao umekuwa ukishambuliwa vikali na majeshi ya Urusi katika siku za hivi karibuni.

Shambulizi la droni lashambulia kinu cha nyuklia Ukraine

Kwenye mahojiano hayo, rais huyo wa Ukraine alisema bado ana matumaini kuwa Ujerumani itaipatia nchi yake makombora ya masafa marefu chapa ya Taurus.

Kansela Olaf Scholz pamoja na baraza la chini la bunge la Ujerumani wamekataa hadi sasa kutuma silaha hizo.