1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy kufanya ziara Ufaransa Alhamis na Ijumaa

5 Juni 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy anatarajiwa nchini Ufaransa kwa ajili ya ziara rasmi hapo kesho Alhamis na Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4geoQ
Singapore I Mkutano wa Usalama Shangri-La Dialogue - Volodymyr Zelenskyj
Volodymyr Zelensky (M), Rais wa Ukraine, akiwasili katika Hoteli ya Shangri-La, ambapo Mazungumzo ya 21 ya Shangri-La yalifanyika.Picha: Vincent Thian/AP/picture alliance

Rais Emmanuel Macron atampokea zelenskiy katika kasri la Elysee. Taarifa kutoka ikulu hiyo imesema kwamba wawili hao wanapanga kujadiliana kuhusu hali ya kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi na mahitaji ya Ukraine. Macron amesema kwamba atatoa tamko kuhusiana na suala la kutumwa kwa wanajeshi wa Ufaransa watakaotoa mafunzo kwa wanajeshi kwa Ukraine nchini humo wakati wa ziara hiyo. Uwezekano wa kuwatuma wanajeshi wa toa mafunzo kutoka nchi za Magharibi huko nchini Ukraine ili kuliunga mkono jeshi la nchi hiyo ni suala ambalo limekuwa likijadiliwa katika siku za hivi karibuni. Lakini hakujakuwa na mipango rasmi kama hiyo ya utoaji mafunzo.