1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya raia 500 waliuawa kwenye mashambulizi Sudan

24 Machi 2026

Zaidi ya raia 500 waliuawa kwenye mashambulizi ya droni nchini Sudan kati ya Januari na Machi 2026.

https://p.dw.com/p/5B1w7
Sudan, Khartoum, vita vya wenyewe kwa wenyewe
Umoja wa Mataifa waelezea wasiwasi kuhusu ongezeko la mashambulizi ya droni katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan Picha: Wang Hao/Xinhua/IMAGO

Umoja wa Mataifa umesema hayo leo Jumanne na kuongeza kuwa mauaji mengi yalitokea katika jimbo la kimkakati la Kordofan.

Shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limesema kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya droni katika vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan.

Msemaji wa shirika hilo Marta Hurtado amewaambia waandishi Habari mjini Geneva kwamba katika wiki mbili za kwanza za Machi pekee, taarifa zilizopokelewa zinaonyesha kuwa zaidi ya raia 277 waliuawa. Zaidi ya robo tatu yao waliuawa katika mashambulizi ya droni.

Aliangazia hasa shambulio la tarehe 20 Machi dhidi ya Hospitali ya El-Daein, katika jimbo la Darfur Mashariki, lililoua watu 70, wakiwemo watoto 13, na kujeruhi wengine 146.