Wickremesinghe achaguliwa rais wa Sri Lanka
20 Julai 2022Matangazo
Kura hiyo inatishia kuchochea msukosuko wa kisiasa katika taifa hilo la kisiwa. Baada ya kura hizo zilizokuwa na ushindani, Wickremesinghe alipata kura 134 huku mpinzani wake mkuu Dulla Alahapperuma akijizolea kura 82.
Mgombea wa tatu, Anura Kumara Dissanayake, alipata kura tatu pekee kutoka kwa chama chake.
Rais wa zamani Gotabaya Rajapaksa alimteua Wickremesinghe kama waziri mkuu mwezi Mei, akitumai uteuzi huo ungeleta utulivu katika nchi hiyo ambayo inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi.
Wickremesinghe alihudumu kama rais wa mpito baada ya Rajapaksa kuikimbia nchi wiki iliyopita na kujiuzulu kwa njia ya barua pepe.