1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaIndia

WHO yatahadharisha dawa ya kikohozi kutoka India

Zainab Aziz
8 Agosti 2023

Shirika la afya duniani, WHO limetoa tahadhari nyingine juu ya dawa ya kikohozi inayotengenezwa nchini India. Shirika hilo limetanabahisha kwamba mchanganyiko wa dawa hiyo ya kunywa unaweza kusababisha madhara.

https://p.dw.com/p/4Utj4
 Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom GhebreyesusPicha: Carsten Koall/dpa/picture alliance

Shirika la afya duniani, WHO limetoa tahadhari nyingine juu ya dawa ya kikohozi inayotengenezwa nchini India. Shirika hilo limetanabahisha kwamba mchanganyiko wa dawa hiyo ya kunywa unaweza kusababisha madhara na hata vifo. Hii ni mara ya tano mnamo muda wa miezi 10, asasi hiyo inatahadharisha juu ya hatari ya dawa hiyo kutoka India.Hali ya maambukizi imekuwa mbaya nchini India

Kwa mujibu wa WHO dawa hiyo imebainika kuwa na sumu. Limesema kiwango duni cha dawa hiyo, inayoitwa Cold Out, ni hatari hasa kwa watoto. Juu ya tahadhari ya shirika la WHO, makamu wa rais wa kampuni inayotengeneza dawa hiyo amesema kampuni yake ilitoa tenda kwa kampuni nyingine na kwamba kampuni yake haijathibitisha kuokekana sumu katika dawa husika baada ya kufanya uchunguzi.