1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

WHO: Zaidi ya watu milioni 2 hawana huduma za afya Darfur

26 Machi 2026

Zaidi ya watu milioni 2 huko Darfur nchini Sudan wameachwa bila huduma muhimu za afya baada ya shambulio la droni la wiki iliyopita kupelekea kusitishwa kwa shughuli katika hospitali kubwa eneo hilo.

https://p.dw.com/p/5B8Lu
Picha ya satelaiti ikionyesha eneo kuliko hospitali huko El Fasher
Picha ya satelaiti ikionyesha eneo kuliko hospitali huko El FasherPicha: Airbus DS/AP Photo/picture alliance

Hayo yameelezwa na Shirika la Afya Duniani WHO na afisa mmoja wa shirika la misaada. Shambulio hilo linalotajwa kuendeshwa na jeshi la Sudan, lilisababisha vifo vya watu 70 na kuharibu  Hospitali ya Al Daein,  ambayo ilikuwa ikiwahudumia watu kote katika jimbo la Darfur Mashariki.

Hayo yakijiri, mapigano yameendelea huku kundi la wanamgambo la RSF likitangaza kuuteka mji wa kimkakati wa Kurmuk, uliopo mpakani mwa Sudan na Ethiopia, huku mamlaka za Chad zikiwazuia wakimbizi wa Sudan kuvuka mpaka wa Al‑Tina, kutokana na sababu za kiusalama.