WHO: Mlipuko wa Ebola, Kongo huenda ulianza muda mrefu
21 Mei 2026
Matangazo
Mtalaamu wa virusi wa shirika WHO Anais Legand amewaambia waandishi habari mjini Geneva kwamba wamefikia hitimisho hilo baada ya kutathmini ukubwa wa mlipuko na namna ugonjwa huo ulivyosambaa.
Hadi sasa inashukiwa watu wengine zaidi ya 600 wameambukizwa ugonjwa wa Ebola ikiwa karibu wiki moja tangu mlipuko wake ulipothibitishwa kwenye jimbo la Ituri, mashariki mwa Kongo.
WHO imesema inatarajia idadi ya visa vya Ebola itaendelea kupanda na maambukizi yanatarajiwa kwenye nchi jirani na Congo. Hata hivyo, shirika hilo limeondoa uwezekano wa mlipuko wa sasa kuwa janga kwa ulimwengu mzima.