Waziri Steinmeier akosoa rushwa nchini Uganda | Matukio ya Afrika | DW | 23.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Waziri Steinmeier akosoa rushwa nchini Uganda

Uganda ni nchi yenye viwango vikubwa mno vya rushwa. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier aliangazia suala hilo wakati alizuru nchini humo mwishoni mwa wiki katika ziara yake ya barani Afrika

Ilichukua muda, lakini serikali ya Uganda na Gauff, kampuni ya kiwango cha wastani yenye makao yake mjini Nuremberg, Ujerumani, wamesaini makubaliano ya mkakati wa ujenzi wa bandari mpya ya Kampala katika eneo la Bukasa. Kampuni hiyo imekuwa ikiutafuta mradi huo tangu mwaka wa 2008.

Muasisi wa kampuni hiyo Helmut Gauff alisema Wajerumani hawakubali rushwa na Waganda wanafahamu hilo. Vinginevyo, mambo yangesonga haraka. Labda ingechukua miaka miwili pekee badala ya mitatu kusaini kandarasi hiyo.

Saini waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier inaipa kandarasi hiyo kiwango fulani cha uzito. Nchini Uganda, kituo cha tatu katika ziara yake ya Afrika, Steinmeier alisema mara si moja kuwa Ujerumani ina matarajio fulani kutoka kwa washirika wake "Kupambana na rushwa - katika nchi nyingi - ni suala ambalo ushiriki zaidi unaweza kutarajiwa." Hata hivyo, nasisitiza kwamba "Mataifa ya Afrika Mashariki ni kanda ambayo Ujerumani na Umoja wa Ulaya wanapaswa kutafuta ushirikiano wa karibu".

Angola Helmut Gauff Fórum Económico alemão-angolano

Helmut Gauff muasisi wa kampuni ya Ujerumani ya Gauff

Kwanza kabisa kabla ya yote, katika vita dhidi ya rushwa, katika nchi nyingi ambazo tunazuru, kuna mengi ya kupendeza kuhusiana na hilo. Hili sio suala la mawazo ya kutamani bali suala la utenda kazi na faida.

Uganda inaorodheshwa ya 142 kati ya 175 kwenye viwango vya nchi fisadi ulimwengu na Shirika la Transparency International. Inasemekana kuwa kila mradi wa miundo mbinu unaoidhinishwa nchini humo kwanza lazima upitie dawati la Rais Yoweri Museveni. Ni yeye anayeamua ni nani anapata mradi huo. Gauff amesema hilo sio kweli – lakini pia akasema mtoto wake wa kiume ana mawasiliano mazuri na rais Museveni. Mbali na hayo, alisema kampuni yake huwekeza katika miradi ya kijamii kama vile taasisi za elimu na makazi ya mayatima.

Bandari ya Kampala katika eneo la Bukasa ina nafasi kubwa ya kujengwa kwa sababu kuna mahitaji ya kweli. Bila hiyo, Uganda ambayo haina njia ya moja kwa moja ya baharini, inaweza tu kuuza nje bidhaa zake kwa kutumia barabara ya Ukanda wa Kaskazini uliojazana kupita kiasi kuelekea bandari ya Mombasa, Kenya.

Bukasa itakuwa chanzo cha barabara mpya ya Ukanda wa Katikati inayofika katika bandari za nchi jirani Tanzania. Huenda ikasababisha mabadiliko makubwa ya kiuchumi katika eneo hilo zima. Huenda – ikiwa rushwa haitabakia kuwa mfano imara kabisa wa kibiashara

Mwandishi: Dagmar Engel/DW
Mtafsiri: Bruce Amani
Mhariri:Josephat Charo

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com