1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu karibu 100 watekwa nyara na wahalifu nchini Nigeria

19 Machi 2024

Watu wenye silaha nchini Nigeria wamewateka nyara takriban watu 100, wakiwemo wanawake na watoto katika mashambulio mawili ya mwishoni mwa jumaa katika jimbo la Kaduna.

https://p.dw.com/p/4dt3P
Nigeria Abuja
Wakaazi wa Kaduna huko NigeriaPicha: Kola Sulaimon/AFP/Getty Images

Watu wenye silaha nchini Nigeria wamewateka nyara takriban watu 100, wakiwemo wanawake na watoto katika mashambulio mawili ya mwishoni mwa jumaa katika jimbo la Kaduna.Wanafunzi wasiopungua 287 watekwa nyara kaskazini mwa Nigeria

Hayo yameelezwa na wakaazi pamoja na msemaji wa polisi huko Kaduna Mansur Hassan aliyethibitisha tukio la Jumapili usiku katika kijiji cha Kajuru Station, bila hata hivyo kutoa idadi kamili ya watu waliotekwa. Tanko Wada Sarkin, mkuu wa kijiji hicho amesema watu 87 ndio waliotekwa.

Utekaji nyara unaofanywa na magenge ya wahalifuambao baadaye hudai fidia, umekuwa tukio la karibu kila siku nchini Nigeria, haswa maeneo ya kaskazini, huku mamlaka za nchi hiyo zikishindwa kukabiliana na vitendo hivyo.