1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Watu wengine 44 waokolewa tetemeko la Taiwan

Josephat Charo
4 Aprili 2024

Wafanyakazi wa uokozi nchini Taiwan wamewaokoa watu wengine 44 ambao walikuwa hawajulikani waliko na kuwapeleka maeneo salama kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea siku ya Jumatano.

https://p.dw.com/p/4eQql
Tetemeko la Taiwan
Helikopta ya wafanyakazi wa uokozi wa Taiwan ikiwa kwenye operesheni za uokozi.Picha: Tyrone Siu/REUTERS

Hayo ni kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Taiwan, Lin You-chang, jioni ya Alkhamis (Aprili 4).

Katika ripoti ya shirika la habari la serikali (CNA), Waziri Lin You-chang alisema watu hao walikuwa wamenasa kwenye njia mbili za chini ya ardhi.

Soma zaidi: Takribani watu 1,000 wajeruhiwa katika tetemeko la ardhi Taiwan

Ripoti hiyo pia ilisema maafisa waliwaokoa watu wengine tisa waliokuwa kwenye pango.

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Taiwan, kufikia sasa maafisa wamewaokoa watu takriban 70 na kuwapeleka katika maeneo salama kufuatia tetemeko hilo la ardhi.

Maafisa bado hawajapata mawasiliano na watu wengine watatu kutoka Canada na Australia, ambao hawajulikani walipo.