1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu wajeruhiwa katika tetemeko la ardhi Taiwan

3 Aprili 2024

Karibu watu 9 wamefariki dunia na wengine 963 kujeruhiwa kutokana na tetemeko la ardhi lililoikumba pwani ya mashariki ya Taiwan leo. Haya yamesemwa na mamlaka ya zima moto ya Taiwan.

https://p.dw.com/p/4eOn4
Taiwan -tetemeko
Athari za tetemeko TaiwanPicha: AFP

Karibu watu 9 wamefariki dunia na wengine 963 kujeruhiwa kutokana natetemeko la ardhi lililoikumba pwani ya mashariki ya Taiwan leo. Haya yamesemwa na mamlaka ya zima moto ya Taiwan.

Mamlaka hiyo inasema jumla ya watu 143 wamenaswa wakiwemo wachimba migodi 71 wa kampuni mbili za sementi na madereva waliokuwa wakiendesha magari katika barabara za chini ya ardhi.

Watu hao walionaswa wote wapo katika mji wa milimani wa Hualien, ambao upo karibu na chimbuko la tetemeko hilo baya zaidi kuwahi kuikumba Taiwan katika kipindi cha miaka 25 na kusababisha uharibifu mkubwa.

Kulingana na mamlaka hiyo ya zima moto, Wajerumani wawili waliokuwa wamenaswa katika barabara moja ya chini wameokolewa. Matetemeko madogo madogo yamerikodiwa katika eneo hilo katika kipindi cha saa nane baada ya tetemeko hilo kubwa.