1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaKenya

Watu wasiopungua 70 wafariki Kenya kufuatia mafuriko

27 Aprili 2024

Mvua kubwa na mafuriko vimesababisha vifo vya watu wasiopungua 70 nchini Kenya kuanzia katikati mwa mwezi Machi.

https://p.dw.com/p/4fFbO
Nairobi 2024 | Mafuriko huko Mathare
Mvua kubwa na mafuriko huko KenyaPicha: Daniel Irungu/EPA

Hayo yameelezwa na msemaji wa serikali Isaac Mwaura, ikiwa ni idadi mara mbili ya ile iliyoripotiwa mapema wiki hii.

Hata hivyo Mwaura alikanusha hapo jana madai kwamba mamia ya watu wamekufa kufuatia mafuriko yanayoendelea nchini humo na kutoa idadi hiyo rasmi ya vifo.

Kwa wiki kadhaa sasa, nchi hiyo ya Afrika Mashariki imekuwa ikishuhudia mvua kubwa iliyosababisha mafuriko katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, na pia katika mikoa ya magharibi na kati.

Mafuriko yaua watu 10 jijini Nairobi Kenya