1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 47 wauawa Syria

Halima Nyanza(ZPR)17 Septemba 2011

Kwa mujibu wa ripoti za wanaharakati wa upinzani, hadi watu 47 waliuawa na vikosi vya usalama vya Syria hapo jana, baada ya waandamanaji kumiminika barabarani katika sehemu mbali mbali nchini humo.

https://p.dw.com/p/12aqv
Machafuko bado yanaendelea SyriaPicha: picture alliance/dpa

Kama raia 21 waliuawa katika wilaya ya Idlib karibu na mpaka wa Syria na Uturuki.

Kwa mujibu wa wanaharakati hao wa upinzani, vikosi hivyo vilikuwa vikifyatua risasi ovyo na wenyeji hawakuweza kuwasaidia majeruhi.

Wengine 6 waliuawa Hama na vifo vingine vilitokea mji mkuu Damascus, Homs na Deir al-Zour.

Syrien YOUTUBE SCREENSHOT HOMS Demonstration Hubschrauber Gewalt
Mji wa homs ambao unalengwa pia na mashambulioPicha: Screenshot youtube

Ripoti hizo haziwezi kuthibitishwa na vyombo huru vya habari kwani serikali ya Syria imewapiga marufuku waandishi wa habari wa kigeni.