1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaQatar

Watu 12 wajeruhiwa baada ya ndege kukumbwa na msukosuko

26 Mei 2024

Watu kumi na mbili wakiwemo abiria sita na wahudumu sita wa ndege wamejeruhiwa baada ya ndege ya shirika la ndege la Qatar Airways iliyokuwa inatoka Doha kwenda Ireland ilipokumbwa na msukomsuko angani.

https://p.dw.com/p/4gITm
Ndege aina ya Boeing 777 ya shirika la ndege la Qatar
Ndege aina ya Boeing 777 ya shirika la ndege la QatarPicha: Urbanandsport/NurPhoto/picture alliance

Watu kumi na mbili wakiwemo abiria sita na wahudumu sita wa ndege wamejeruhiwa baada ya ndege ya shirika la ndege la Qatar Airways iliyokuwa inatoka Doha kwenda Ireland ilipokumbwa na msukomsuko angani.

Katika taarifa, mamlaka inayosimamia uwanja wa ndege wa Dublin imesema, timu ya uokoaji na huduma za dharura ikiwa ni pamoja na polisi wa uwanja wa ndege na idara ya zimamoto iliwasili pindi tu ndege hiyo ilipotua.

Soma pia: Msukosuko wa ndege wasababisha kifo cha mtu mmoja 

Licha ya msukosuko huo, mamlaka hiyo imeeleza kuwa ndege hiyo imetua salama na imewasili kwa wakati kama ilivyopangwa.

Tukio hilo limetokea siku tano tu baada ya ndege ya shirika la ndege la Singapore iliyokuwa inatokea London kwenda Singapore, ilipolazimika kutua mjini Bangkok kutokana na msukosuko mkubwa angani na ambao ulisababisha kifo cha mzee wa miaka 73 raia wa Uingereza na kuwaacha abiria wengine 20 katika uangalizi maalum wa madaktari.