1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSingapore

Msukosuko wa ndege wasababisha kifo cha mtu mmoja

21 Mei 2024

Mtu mmoja amekufa na wengine 30 wamejeruhiwa katika mtikisiko mkubwa wakati wa safari ya ndege ya shirika la Singapore Airlines kutokea London kuelekea Singapore.

https://p.dw.com/p/4g6zN
Thailand Bangkok 2024 | Singapur Airlines Maschine | Notlandung am Flughafen
Picha: REUTERS

Data kutoka kwa kituo cha kufuatilia safari za ndege FlightRadar24 zimeonesha kuwa ndege hiyo ilishuka ghafla kwa mita 1,800 katika anga la pwani ya magharibi ya Myanmar.

Msimu wa mvua umeanza katika eneo hilo na kumekuwa na mvua kubwa katika maeneo mengi ya kanda hiyo.

Ndege aina ya Boeing chapa 777-300ER iliondoka London Jumatatu na ikakumbwa na msukosuko mkali ikiwa njiani na kulazimika kuelekezwa hadi Bangkok nchini Thailand ambako imetua leo mwendo wa saa nane kasorobo.

Mlikuwa na abiria 211 na wafanyakazi 18 ndani ya ndege hiyo.

Shirika la Singapore Airlines limetoa rambirambi kwa kwa familia ya abiria aliyekufa na limesema linashirikiana na maafisa wa Thailand kutoa msaada wa matibabu huku timu yake ikiwa njiani kuelekea Bangkok.