1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

UNICEF: Watoto 68,000 wanahitaji msaada wa kiutu Nepal

Sudi Mnette
12 Februari 2024

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema watoto wapatao 68,000 na familia zao ambao walinusurika kwenye tetemeko la ardhi wanahitaji msaada wa kiutu.

https://p.dw.com/p/4cHFa
Tetemeko la ardhi la Nepal
Baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.4 kupiga eneo la magharibi mwa Nepal, watu wengi walikufa na wengine wengi kujeruhiwa.Picha: picture alliance/dpa/ZUMA Press Wire

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema watoto wapatao 68,000 na familia zao ambao walinusurika kwenye tetemeko baya zaidi la ardhi kutokea Nepal katika kipindi cha takribani miaka minane iliyopita wanahitaji msaada zaidi wa kibinadamu ili kustawisha upya maisha yao. Shirika hilo limesema ikiwa imetimia siku 100 baada ya tetemeko hilo ambalo takriban watu 200,000 wakiwemo watoto 68,000. wanakabiliwa na baridi kali katika makazi ya muda. Na wengi wao wenye kukabiliana na baridi wakihitaji msaada wa kiutu. Shirika la Umoja wa Mataifa limetoa himizo la ombi la mchango wa dola milioni 14.7 kikiwa kiwango mahususi cha fedha za kusaidia watoto hao. Novemba 3, tetemeko la ardhi la kiwango cha 6.4 katika kipimo cha richter lilikumbawilaya mbili za Jajarkot na Rukum katika eneo la magharibi la Himalaya na kuua takrian watu 154, nusu ya hao wakiwa ni watoto.