1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapinzani waazimia kufanya maandamano Kenya.

11 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CoHH

NAIROBI.

Baada ya juhudi za kimataifa kushindikana katika kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Kenya wapinzani wametoa mwito wa kufanyika maandamano.Kiongozi wa chama cha upinzani Raila Odinga amesema serikali haijaonesha dhamira ya kuutatua mgogoro huo.

Hatahivyo rais Kibaki na bwana Odinga wanalaumiana juu ya kushindikana kwa juhudiza kuleta upatanishi.