1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UgaidiAustralia

Watu 7 wakamatwa wakihusishwa na washambuliaji wa Bondi

19 Desemba 2025

Wanaume saba wanaoaminika kuwa na uhusiano wa kiitikadi na washambuliaji wawili waliohusika na shambulizi la kigaidi kwenye ufuo wa Bondi siku ya Jumapili wamekamatwa kusini-magharibi mwa Sydney.

https://p.dw.com/p/55g8a
Australia Sydney 2025 | Jumuiya ya Bondi wakitoa heshima zao kuwakumbuka walioarthirika na shambulizi la risasi, Bondi, Sydney
Jumuiya ya Bondi wakitoa heshima zao kuwakumbuka walioarthirika na shambulizi la risasi kwenye ufukwe wa Bondi mnamo Desemba 19, 2025 huko Sydney, Australia.Picha: Cameron Spencer/Getty Images

Taarifa hiyo imetolewa na kituo cha utangazaji cha ABC nchini Australia siku ya Ijumaa.

Polisi wa New South Wales wamewakamata wanaume hao katika kitongoji cha Liverpool huko Sydney jana Alhamisi, wakitokea jimbo jirani la Victoria wakitumia magari mawili.

Naibu Kamishna wa Polisi wa NSW David Hudson aliiambia ABC Sydney kwamba kulikuwa na "ishara fulani kwamba Bondi lilikuwa ni moja ya  maeneo ambayo huenda waliyatembelea.

Waziri mkuu wa Australia mapema leo ametangaza mpango wa kitaifa wa kununua tena bunduki ili kuziondoa silaha nzito kufuatia mauaji hayo yaliwaua watu 15 na kuwajeruhi wengine kadhaa.