Wanatarajiwa kushuhudia zoezi la kuharibu kituo cha kufanya majaribio ya Nyuklia huko Korea Kaskazini,zoezi ambalo wataalamu wa Nyuklia hawakualikwa.Waandishi habari waliokwenda ni pamoja na kutoka Korea Kusini. Hatua hii imekuja baada ya Korea Kaskazini kufuta mkutano na Korea Kusini huku pia ikitishia kwamba kiongozi wake Kim Jong Un hatoshiriki mkutano pamoja na rais wa Marekani Donald Trump.