Wahamiaji 11 wafa maji Libya | Matukio ya Afrika | DW | 26.10.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Wahamiaji 11 wafa maji Libya

Kiasi wahamiaji 11 ikiwemo mwanamke mjamzito waliojaribu kuingia barani Ulaya wamekufa Jumapili baada ya boti waliyokuwa wakitumia kuzama karibu na pwani ya Libya,

(Picha ya maktaba)

(Picha ya maktaba)

Kisa hicho ni cha tatu ndani kipindi cha wiki moja.

Hayo yameelezwa na shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM, ambalo msemaji wake Safa Msehli, amearifu kuwa wavuvi na walinzi wa pwani ya Libya walifanikiwa kuwaokoa takribani wahamiaji wengine 10.

Jumanne iliyopita karibu wahamiaji 15 walikufa baharini baada ya boti yao kuzama na wengine watano walikufa siku ya Alhamisi kwa sababu kama hiyo.

Ndani ya mwaka huu, wahamiaji 500 wamekufa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania ili kuingia Ulaya na shirika la IOM limeonya kuwa huenda idadi ni kubwa kwa sababu vifo vingine havijajumuishwa.