1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Wafanyabiashara wagoma Kampala

8 Aprili 2024

Mji mkuu wa Uganda Kampala umetikiswa na mgomo wa wafanyabiashara. Mgomo huo umetatiza shughuli za kawaida katika mji huo siku ya Jumatatu.

https://p.dw.com/p/4eYTA
Uganda Kampala | Maduka yaliyofungwa mjini Kampala kufuatia mgomo wa wafanyabiashara
Maduka yaliyofungwa mjini Kampala kufuatia mgomo wa wafanyabiasharaPicha: Lubega Emmanuel/DW

Wafanyabiashara wameyafunga maduka yao wakipinga mienendo ya mamlaka ya mapato kuwapandishia ushuru kwa bidhaa mbalimbali hasa zile zinazoagizwa kutoka nje ya Uganda.

Watu wanaoendesha shughuli zao katikati ya mji hasa wafanyakazi kwenye biashara mbalimbali wamejikuta katika adha kubwa walipokuta wenye maduka wakiwa wameyafunga.

Waliwaagiza kurudi nyumbani lakini wengi walikataa wakisema kuwa wao huchuma riziki ya kila siku na hawawezi kurudi nyumbani bila chochote.

Vyombo vya usalama vyadhibiti mji

Miongoni mwa walioathrika na mgomo huu ambao umeongozwa na wenye maduka ya jumla ni wale wanaobeba mizigo pamoja na bodaboda katika kitovu cha mji.

Uganda Kampala | Umwelt | Kampf gegen Altkleider
Duka la kuuza mitumba katika siku za kawaida za biashara kabla mgomo wa JumatatuPicha: Badru Katumba/AFP

Kadri idadi ya watu ilipongezeka ili hali hawana kinachowashughulisha vyombo vya usalama viliamua kuchukua udhibiti wa mji na kuweka doria kwenye barabara zote. Serikali imewahimiza wafanyabaishara wafungue maduka huku ikijadili kero yao.

Lakini baadhi ya wenye maduka hasa wale wa kigeni walihofia kuwa wanaweza kunyanyswa na wenyeji licha ya kuhakikishiwa usalama. Kinachowakera wafanyabaishara ni mienendo ya mamlaka ya mapato kuwapandishia kodi na ushuru hasa kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.

Kisha kuna suala la kuwalazimisha kutoa risiti za mtandaoni ambazo mamlaka hiyo inaweza kufuatilia kukadiria mapato yao na kuwatoza kodi ya mauzo na ile ya ongezeko la thamani.

Serikali inatakiwa ijue kuwa shughuli zetu zikitatizwa na hali hii ya kodi basi haiwezi kupata kodi inayotaka

Mgomo wakati wa maandalizi ya Eid

Kitovu cha mji wa kampala ndiko shughuli nyingi za biashara hufanyika. Wafanyabiashaara kutoka mataifa jirani huja kununua bidhaa kwenye maduka ya jumla na hii leo wengi wamejikuta wamekwama na hawajui mgomo huo utachukua muda gani.

Bangladesch Islam l Eid-ul-Fitr, Fest des Fastenbrechens in Dhaka
Mgomo umekuja wakati wa shamra shamra za maandalizi ya EidPicha: Rehman Asad/NurPhoto/picture alliance

Mgomo huu umeanza wakati waumini wa kiIslamu wakijiandaa kwa sherehe za Iddul fitri ambapo manunuzi ni makubwa.

"Sasa maduka yakiwa yamefungwa hatuna budi kubaki na kile tulicho nacho," alisema Jamal Ahmad mteja.

Hadi wakati wa kuandaa taarifa hii wizara ya fedha na mamlaka ya mapato hawajatoa taarifa rasmi ya mwitikio kwa mgomo huu.