1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi 10 wauwawa mashariki mwa Kongo

10 Mei 2021

Wakati hali ya dharura katika mikoa ya Kivu ya Kaskazini pamoja na Ituri inaingia siku yake ya tano tangu kutangazwa na rais wa Tshisekedi, wanajeshi wa DRC wamekabiliana na waasi wa ADF katika mji mdogo wa Halungupa.

https://p.dw.com/p/3tC1F
Demokratische Republik Kongo | Unruhen in Beni
Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Taarifa zinasema kwamba waasi kumi waliuawa na silaha zao sita kukamatwa na jeshi. Na wakati huo huo, kuna ujumbe wa jeshi la Uganda uliowasili Beni,katika maandalizi ya operesheni za pamoja kati ya jeshi la Uganda na lile la Kongo.

"Tumeona na kuhesabu maiti kumi ya wapiganaji wa ADF na kukamata silaha ya kawaida AK-47," alisema Meleki Mulala, msemaji wa jeshi la Kongo.

Mafanikio hayo ya majeshi ya Kongo dhidi ya waasi wa ADF, yamepokelewa kwa shangwe kubwa na mashirika ya kiraia ya Sekta ya Ruwenzori kwa namna ya pekee na yale ya wilaya na mji wa Beni kwa ujumla.

Majeshi ya Kongo yanasema yana uwezo wa kupambana na ADF

Akizingumza na DW, baada ya kuona maiti za waasi wa ADF kumi waliouawa Halungupa, Meleki Mulala, mwenyekiti wa mashirika ya kiraia maarufu Nouvelle société civile katika sekta ya Ruwenzori,pamoja na kushangaa kuona miili ya ADF, anawaomba wakaazi kuliunga mkono kikamilifu jeshi la Kongo,ili kuhakisha kwamba amani ya kudumu inarudi katika Sekta ya Ruwenzori. Huyu hapa Meleki Mulala.

Demokratische Republik Kongo | Präsident Felix Tshisekedi
Rais Felix TshisekediPicha: Arsene Mpiana/AFP/Getty Images

Waasi wa ADF wakiwa kabla na baada ya kutangazwa kwa hali ya dharura na rais Tshisekedi wanaendelea kuvishambulia vijiji, kuwauwa watu pamoja na kupora mali, majeshi ya Congo nayo yanasema kwamba yako na uwezo wa kupambana na ADF hadi pale watatokomezwa, jambo ambalo yanasema litaleta amani ya kudumu kurudi katika eneo hili. kama anavyosema luteni.

"Tumejipanga sawawa ili tusonge mbele na kuwatokomeza hawa watu. Lengo letu nikurudisha amani kwa nguvu ili amani hiyo tuwapatie raia wetu, ili raia wa Beni wajisikie huru kuishi katika eneo ambalo munapatikana amani ya kudumu," alisema Anthony Mualushayi, msemaji wa FARDC jeshi la Congo katika eneo la Beni na Butembo.

Jeshi la Kongo limefanikiwa kuwauwa waasi zaidi ya ADF

Na huko hayo yakiwa namna hiyo,ujumbe wa jeshi la wananchi wa Uganda UPDF, ukiongozwa na meja jenerali Kayandji Muhonga, kamanda wa kitengo cha jeshi linalo uzoefu wakupigana katika mlima na misitu.

DRK Symbolbild FARDC
Wanajeshi wa FARDCPicha: Alain Wandimoyi/AFP

Pamoja na kwamba ujumbe huo haukuzungumza na wanahabari, lakini duru karibu na jeshi la Congo zadokeza, kuwa ziara hiyo ni katika maandalizi ya operesheni za pamoja, baina ya jeshi la Congo na Uganda, ili kuwashinda waasi kutoka Uganda ADF, wanaobebeshwa lawama ya mauwaji ya ma elfu ya wakaazi, kwa kuwakata kwa mapanga.

Na katika kipindi cha myezi minne,majeshi ya serikali ya Congo yameshafanikiwa kuwauwa ADF zaidi ya mia moja, na kuwakamata zaidi ya hamsini,kwa mjibu wa duru toka mashitrka ya kutetea haki za binaadamu, yanayofuatilia kwa karibu operesheni hizo dhidi ya ADF.