1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel iko mbioni kufanya majadiliano ya serikali ya pamoja

Amina Mjahid
6 Aprili 2020

Vyama viwili vinavyoongoza Israel vimefanya majadiliano bila mapumziko katika harakati za kupata makubaliano ya kuunda serikali ya muungano kuelekea wiki moja ya sikukuu ya Kiyahudi ya Pasaka inayoanza Jumatano jioni.

https://p.dw.com/p/3aYNP
Israel Netanjahu und Gantz
Picha: AFP/G. Cohen-Magen

Duru zinaarifu kuwa chama cha buluu na nyeupe kitajiunga katika serikali ya muungano na chama cha Likud chake Waziri Mkuu wa muda Benjamin Netanyahu iwapo chama cha Likud kitatetea demokrasia na kuungana katika juhudi za kupambana na janga la corona.

Kitu ambacho kinajadaliwa pia ni iwapo chama hicho kitakubali msisitizo wa Netanyahu kuhusiana na Israeli kuongeza uhuru wa Israel katika sehemu ya asilimia thelathini ya ukingo wa Magharibi.

Duru nyengine ya chama hicho inasema Netanyahu anataka unyakuzi wa eneo hilo uanze mara moja.