1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUbelgiji

Von der Leyen atetea nia ya kushirikiana na mrengo wa kulia

25 Mei 2024

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der Leyen kwa mara nyingine amejibu ukosoaji unaoipinga nia yake ya kushirikiana na makundi ya mrengo wa kulia katika Bunge la Ulaya.

https://p.dw.com/p/4gHUd
Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya, Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya, Ursula von der Leyen atetea uamuzi wake wa kushirikiana na vyama vya mrengo wa kulia licha ya upinzaniPicha: Mohamed Azakir/REUTERS

Von der Leyen amekiambia kituo cha radio cha Ujerumani cha Deutschlandfunk kwamba atashirikiana na pande zote za kidemokrasia na wanasiasa, bila kujali makundi waliyopo bungeni.

Amesisitiza kuwa vigezo vyake ni kwamba wabunge anaotaka kufanya nao kazi ni wale wanaoiunga mkono Ulaya, wanaoiunga mkono Ukraine katika vita dhidi ya Urusi na wanaoamini katika utawala wa sheria.

Kiongozi huyo, kwa mara ya kwanza alikosolewa mwezi Aprili baada ya kushindwa kuamua juu ya ushirikiano na kundi la wabunge wa mrengo wa kulia la ECR, linalojumuisha chama cha siasa za mrengo wa kulia cha Brothers of Italy, anachotoka Waziri Mkuu wa Italia Georgia Meloni.