1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz amuonya von der Leyen kuhusu vyama vya itikadi kali

25 Mei 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amemuonya Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen dhidi ya kushirikiana na vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia kutafuta muhula wa pili.

https://p.dw.com/p/4gGs1
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Franc Zhurda/AP/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amemuonya Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, kutojaribu kutafuta muhula wa pili madarakani baada ya uchaguzi wa bunge la Ulaya, kwa msaada wa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia.

Scholz amesema ni wazi kuwa uundwaji wa halmashuri kuu ijayo haupaswi kutegemea wingi wa bungeni unaohitaji uungaji mkono wa wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia, na kuelezea masikitiko yake juu ya utata wa baadhi ya matamko ya kisiasa yaliosikika hivi karibuni.

Soma pia:Wahafidhina Ulaya kumuidhinisha von der Leyen muhula wa pili 

Mnamo mwezi Aprili von der Leyen alikataa kuondoa uwezekano wa kushirikiana na kundi la wahafidhina wa mrengo wa kulia na wanamageuzi, ECR, ambalo linahusisha chama cha waziri mkuu wa Italia Georgina Meloni cha Brothers of Italy.

Ubelgiji Brussels | Rais wa Halamashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen anawania muhula wa pili katika wadhifa huo baada ya uchaguzi wa bunege la Ulaya.Picha: Jonathan Raa/NurPhoto/picture alliance

Von der Leyen alitetea uamuzi wake katika bunge la Ulaya siku ya Alhamisi, akisema alishirikiana vyema na Georgina Meloni katika Baraza la Ulaya kama ilivyokuwa na wakuu wengine wa nchi na serikali.

Scholz amesema msimamo wake wa wazi ni kwamba itawezekana tu kuunda urais wa halmashauri kuu kupitia vyama vya jadi, na jambo lolote lingine litakuwa kosa kwa mustakabali wa Ulaya.