1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Vikosi vya Urusi vinapata mafanikio Ukraine, asema Putin

16 Oktoba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin, amedai kwamba vikosi vyake vimefanikiwa kuimarisha uwezo wao katika maeneo ya mapambano nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4XZBB
Putin amedai vikosi vyake vimepata mafanikio katika maeneo kadhaa nchini Ukraine
Putin amedai vikosi vyake vimepata mafanikio katika maeneo kadhaa nchini UkrainePicha: Pavel Bednyakov/REUTERS

Akizungumza na kituo cha televisheni cha nchini Urusi jana Jumapili, Putin amesema vikosi vyake vimepata mafanikio katika maeneo kadhaa, ikiwemo katika mji wa mashariki wa Avdiivka unaokabiliwa na mzozo.

Hayo yakijiri, ripoti ya intelijensia ya Uingereza imesema, Urusi inajenga njia mpya ya reli kuelekea mji unaokaliwa wa Mariupol.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa Urusi inatumia njia hiyo kusafirisha risasi, silaha zaidi, mafuta na wanajeshi hadi Ukraine.

Hata hivyo, ripoti imesema njia hiyo mpya inayojengwa na wanakandarasi wa kiraia, kuwakomboa wanajeshi wa Urusi mahali pengine, iko ndani ya eneo ambalo mifumo ya makombora marefu ya Ukraine inafikia.