Vifo kutokana na Ebola DRC vyafikia 180 | Matukio ya Afrika | DW | 02.11.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Vifo kutokana na Ebola DRC vyafikia 180

Watu 180 wamefariki katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na mripuko wa Ebola. Wizara ya Afya yasema

Mripuko wa ugonjwa wa Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umesababisha vifo vya watu 180, kulingana na wizara ya afya nchini humo. Kuna vifo kumi ambavyo vimetokea katika siku za hivi karibuni. Wizara ya Afya ilisema jana Alhamisi kuwa imesajili visa 285 vinavyoweza kuthibitika kuwa Ebola na vifo 180. Mripuko wa hivi karibuni unasambaa kwa kasi katika eneo linalokumbwa na machafuko la Kaskazini mashariki jimbo la Kivu Kaskazini ambayo ni makao ya makundi yenye silaha. Mripuko wa hivi karibuni ni wa 10 tangu mripuko wa kwanza nchini humo kutokea mwaka 1976. Tangu mpango wa chanjo ulioanza mwezi Agosti, zaidi ya watu 25,000 wamepata chanjo.