1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Venezuela yasitisha shughuli za ofisi ya haki za binadamu

Sylvia Mwehozi
16 Februari 2024

Mamlaka nchini Venezuela zimesitisha shughuli za ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na kuamuru wafanyakazi wake kuondoka ndani ya saa 72.

https://p.dw.com/p/4cSQZ
Venezuela
Rais wa Venezuela Nicolas MaduroPicha: Matias Delacroix/AP/picture alliance

Mamlaka nchini Venezuela zimesitisha shughuli za ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na kuamuru wafanyakazi wake kuondoka ndani ya saa 72.

Uamuzi huo unakuja siku chache tu baada ya mamlaka kumkamata mwanaharakati mashuhuri Rocio San Miguel. Umoja wa Mataifa ulielezea wasiwasi wake mkubwa juu ya kukamatwa kwa mwanaharakati huyo siku mbili tu zilizopita na kutaka "kuachiliwa mara moja."

Soma: UN: Venezuela iliwaua raia kinyume cha sheria

Waziri wa mambo ya nje  wa Venezuela Yvan Gil ameishutumu ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa kuchukua jukumu lisilofaa na kwamba imekuwa kampuni ya kisheria ya wapangaji wa mapinduzi na magaidi wanaofanya njama za kudumu dhidi ya nchi hiyo.

Msemaji wa ofisi hiyo ya haki za binadamu ambayo imekuwepo Venezuela tangu 2019  Ravina Shamdasani, alisema wanatafakari tangazo hilo na kutathmini hatua zinazofuata.