1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Venezuela wapiga kura kumchaguwa mpinzani wa Maduro

22 Oktoba 2023

Raia wa Venezuela wanapiga kura kumchagua mgombea mmoja wa upinzani atakayepimana nguvu na Rais Nicolas Maduro katika inkyang'anyiro cha urais mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/4XrvY
Upinzani nchini Venezuela wasaka mgombea mmoja wa kukabiliana na Rais Nicolas Maduro.
Upinzani nchini Venezuela wasaka mgombea mmoja wa kukabiliana na Rais Nicolas Maduro.Picha: Ariana Cubillos/AP/picture alliance

Uchaguzi huo wa siku ya Jumapili (Oktoba 22) ulifanyika wakati Marekani ikitowa ahadi ya kuiwekea vikwazo nchi hiyo iwapo serikali itashindwa kuondoa marufuku inayowabana baadhi ya wanasiasa wa upinzani kushikilia nafasi za serikali. 

Maria Corina Machado, aliye na miaka 56, mhandisi na mbunge wa zamani alitajwa kuongoza kwa alama 40 mbele ya wapinzani wake.

Soma zaidi: Marekani kulegeza vikwazo vya mafuta na gesi dhidi ya Venezuela

Lakini Machado kama ilivyokuwa kwa waliokuwa wapinzani wawili wa Maduro, haruhusiwi kushikilia nafasi katika ofisi za umma kufuatia kuunga mkono vikwazo ilivyowekewa serikali ya Maduro na Marekani na hataweza kujisajili kushiriki uchaguzi mkuu. 

Soma zaidi: Serikali, upinzani Venezuela wakubaliana uchaguzi mwakani

Machado aliyesema lengo lake ni kumshinda Maduro katika uchaguzi ulio  huru, haki na wa amani, akisisitiza kuwa anaweza kuishinikiza tume ya uchaguzi kumuacha ajisajili.

Rais Maduro hajatangaza nia yake ya kugombea, lakini waangalizi wengi wanamtarajia kufanya hivyo.