1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vatican yafananisha kubadilisha jinsia na kutoa mimba

Mohammed Khelef
9 Aprili 2024

Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani yametangaza kwamba operesheni za kubadilisha jinsia na kubeba mimba ya watu wengine ni kinyume na ubinaadamu, na ni sawa na utoaji mimba na kusaidia watu kufa.

https://p.dw.com/p/4eYxY
Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis.Picha: Andrew Medichini/AP Photo/picture allliance

Kanisa hilo lilisema siku ya Jumatatu (Aprili 8) kuwa mambo yanakinzana na matakwa ya Mungu kwenye maisha ya mwanaadamu.

Tamko hilo la Vatican lenye kurasa 20 lililotolewa baada ya mapitio ya zaidi ya miaka mitano na kuthibitishwa na Mkuu wa Kanisa hilo, Papa Francis, tarehe 25 Machi na kisha kuagiza kuwa lichapishwe na kusambazwa.

Soma zaidi:  (SW): Vatican yafanani... Vatican yaendelea kupinga kubadilisha jinsia

Kwa kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki, ambaye alikuwa anachukuliwa kama mwenye msimamo wa wastani na anayefanya juhudi kubwa ya kuwafikia watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, tamko hili lilipokelewa na jamii hiyo kama pigo kubwa.