1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden na Trump wamewaumiza zaidi Wamarekani

16 Aprili 2024

Watifiti nchini Marekani wanaeleza sababu za kwa nini Rais Joe Biden na mtangulizi wake Donald Trump wanashambuliana, Wengi wanasema wanasiasa hao wamefanya mambo yaliyowaumiza wamarekani zaidi kuliko mema kwa nchi .

https://p.dw.com/p/4eqg3
Joe Biden vs Donald Trump
Picha: imago images

Wote Biden na Trump wanatajwa kuwaumiza wamarekani kwenye masuala muhimu ikiwemo ya uchumi na suala nyeti la uhamiaji, ambalo kwa sasa linachukuliwa kama miongoni mwa karata kwa wawili hao kuisaka Ikulu ya White House.

Kura mpya zilizotolewa na Shirika la habari la AP na Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Umma AP-NORC zimebainisha kwamba zaidi ya nusu ya watu wazima nchini Marekani wanafikiri kuwa kipindi cha utawala wa Rais Biden Biden kimewaumiza zaidi hasa katika masuala ya uhamiaji na kupanda kwa gharama za maisha.

Wakati huo huo, nusu ya wengine wanadhani kuwa wakati wa Rais Trump uliwaumiza wamarekani zaidi hasa kwenye masuala yanayohusu haki za kupiga kura na usalama wa uchaguzi, mahusiano na nchi za nje, sheria za utoaji mimba na mabadiliko ya hali ya hewa.

Soma pia:Donald Trump na msururu wake wa mashtaka mahakamani

Akiwasilisha utafiti huo, Linley Sanders ambaye ni mwandishi wa shirika la habari la AP amesema Kura mpya zilizotolewa na Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Umma cha AP NORC zimegundua kwamba Wamarekani kwa ujumla wanafikiri kwamba wakati wa urais wao, Biden na Trump waliwaumiza zaidi wamarekani kuliko mema katika masuala mbalimbali muhimu.

"Hata hivyo,masuala yote hayo hayafanani kwa wagombea wote wawili," alisema Sanders.

Kura hii ya maoni inasisitiza juu ya kwa nini masuala fulani kama vile utoaji mimba kwa Rais Biden na suala la uhamiaji kwa Trump yamepewa kipaumbele kikubwa kwenye kampeni zao.

Donald Trump mara kwa mara amesikika akiukosoa utawala wa rais Biden huku akisema kwamba utawala huo umeruhusu idadi kubwa ya waomba hifadhi nchini humo.

Na Biden naye amekuwa akitumia majukwaa mbalimbali kumjibu Trump huku akimkosoa rais huyo wa zamani juu ya masuala ya utoaji wa mimba ambayo hivi karibuni mahakama ya juu ya Arizona ilitoa uamuzi wa kuharamisha utaratibu huo.

Trump katika masuala ya demokrasia na kisheria

Akiendelea kuwasilisha utafiti huo Linley Sanders, amesema Trump alikuwa ukingoni kulitumbukiza taifa hilo linalotazamwa kama kinara wa demokrasia kwenye hatari kubwa.

New York, Marekani | Siasa | Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald TrumpPicha: TIMOTHY A. CLARY/AFP

Aliongeza kuwa takriban nusu ya Wamarekani wanasema aliidhuru nchi juu ya haki za kupiga kura na uhusiano wa usalama wa uchaguzi na mataifa ya kigeni.

"Sheria za utoaji mimba na mabadiliko ya hali ya hewa." Linsley alisema ni miongoni mwa mambo ambayo yaliyumba katika utawala wa Trump.

Soma pia:Trump ataka mdahalo wa uchaguzi na Biden

Aliendelea kueleza kuwa Wamerekani walipoulizwa kuchagua kati ya rais aliyewasaidia zaidi, "takriban theluthi moja wanasema Donald Trump na karibu robo moja wanasema Joe Biden. Hata hivyo asilimia 30 ya watu wazima wanasema hakuna rais aliyewanufaisha."

Takwimu hizo zinaonyesha ni jinsi gani ambavyowapiga kura wengi nchini Marekani wamekuwa wamekatishwa tamaa hasa kuelekea uchaguzi mkuu na viongozi hao wawili ambao wanatarajiwa kugombea tena katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Biden katika mfumko wa bidhaa na vita ulimwenguni

Baada ya janga la Uviko-19, Biden aliupaisha uchumi kwa kutoa ajira zaidi ya milioni 15, lakini masuala ya ugavi, vita vya Urusi nchini Ukraine na mfuko wa misaada wa Biden yanatajwa kupandisha gharama za maisha kwa wamarekani na hali hiyo imemuweka kwenye minong'ono ya wamerakani wengi.

Washington, Marekani |Rais Joe Biden
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Greg Nash/AFP/Getty Images

Theluthi moja tu ya Wanademokrat wanafikiri kuwa utawala wa Biden ulisaidia kupunguza gharama ya maisha. Takriban wanademokrasia 3 kati ya 10 wanafikiria urais wa Biden

umesaidia juu ya uhamiaji na usalama wa mpaka ingawa suala hilo limekuwa na ukosoaji mkubwa.

Soma pia:Kinyang´anyiro cha ´Jumanne Kuu´ chawadia Marekani

Suala muhimu kwa wote Biden na Trump kwa ujumla ni kutengeneza ajira, wapo wanaosema kuwa Biden amesaidia kwa asilimia 36 kupatikiana kwa ajira huku watu 4 kati ya 10 wakisema kwamba utawala wa Trump ulisaidia kupunguza gharama za maisha.

Kura hizi za maoni ya watu wazima 1,204 ilifanyika  kati  ya Aprili 4-8, 2024.