1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Kongo wadai kuchezewa ´rafu` kuelekea uchaguzi

15 Desemba 2023

Wakati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inapokaribia kuandaa uchaguzi mkuu wiki ijayo, upinzani na waangalizi huru wametahadharisha juu ya masuala ambayo huenda yakatishia uhalali wa matokeo.

https://p.dw.com/p/4aBiw
Raia wa Kongo akipiga kura wakati wa uchaguzi wa mwaka 2018
Wakongomani watapiga kura Disemba 20, kuchagua rais mpya, wabunge na madiwani.Picha: Stefan Kleinowitz/Zumapress/picture alliance

Upinzani umeeleza wasiwasi wao kuhusu wagombea kuzuiwa kufanya kampeni, uchelewashaji wa orodha kamili ya wapiga kura na kadi za kura zisizosomeka.

Mvutano umeongezeka kuelekea wiki za mwisho za kampeni kabla ya uchaguzi wa Disemba 20. Rais Felix Tshisekedi amelalamikia kile alichokiita "uwanja usiokuwa sawa" na kuzituhumu mamlaka kwa kupanga njama ya kuchakachua matokeo.

Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi ya Kongo, CENI, imekanusha madai hayo.

CENI pia imepinga ukosoaji dhidi yake kwa kushindwa kuandaa uchaguzi ulio huru na wa haki kama ilivyoahidi, licha ya changamoto ya usafirishaji wa vifaa vya kura hiyo katika taifa hilo la pili kwa ukubwa barani Afrika.