1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Indien Rana Ayyub
Picha: Chandan Khanna/Getty Images/AFP

UN wataka mashambulizi dhidi ya mwanahabari India yakomeshwe

John Juma
22 Februari 2022

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wametaka kukomeshwa kwa mashambulizi ya mitandaoni dhidi ya waandishi wa habari wa kike ambao ni Waislamu na wenye asili ya kihindi.

https://p.dw.com/p/47QwS

Wataalam hao wametaka pia maafisa kuchunguza visa hivyo vya dhuluma.

Rana Ayyub ambaye ni mkosoaji mkubwa wa Waziri Mkuu Narendra Modi na serikali yake ya kizalendo chini ya chama cha Bharatiya Janata (BJP), amekuwa akishambuliwa mitandaoni kwa matusi na hata kupokea vitisho vya kuuawa na kubakwa.

Yeye ni mlengwa na mwathiriwa wa kampeni ya mashambulizi na vitisho vinavyoendelezwa na makundi ya kizalendo yenye siasa kali za mrengo wa kulia. Hayo ni kulingana na wachunguzi maalum ambao hawazungumzi kwa niaba ya Umoja wa Mataifa- lakini wana wajibu wa kuripoti matukio hayo. Taarifa iliyotolewa Jumatatu ilieleza hayo.

Mzozo kuhusu zuio la kuvaa hijab India waongezeka

Wamesema mashambulizi dhidi ya Ayyub yalichochewa na makala aliyoandaa kuhusu masuala yanayowaathiri Waislamu wachache wenye asili ya Kihindu, ukosoaji wake dhidi ya serikali kuhusu namna inavyoshulighulikia janga la Covid-19, na maoni yake ya hivi karibuni kuhusu marufuku ya hijab shuleni katika jimbo la kusini, Karnataka.

Waandishi wengine wa habari pia wameelezea hali ya kuongezeka kwa dhuluma dhidi yao chini ya utawala wa Modi na mashambulizi ya mitandaoni dhidi yao.
Waandishi wengine wa habari pia wameelezea hali ya kuongezeka kwa dhuluma dhidi yao chini ya utawala wa Modi na mashambulizi ya mitandaoni dhidi yao.Picha: Nicolas Asfouri/AFP/Getty Images

Wataalam hao waliongeza kuwa serikali ya India imeshindwa kulaani au kuchunguza mashambulizi hayo. "Amekuwa mwathiriwa wa dhuluma kutoka kwa maafisa wa serikali kwa sababu ya ripoti anazoangazia,” wamesema wataalam hao na kuongeza kuwa miongoni mwa dhuluma hizo ni kufungwa kwa akaunti yake ya benki na kukamatwa kwa mali zake nyingine.

Ayyub mwenye umri wa miaka 37 amejikita katika uanahabari wa upekuzi na ameandika kitabu kinachomshutumu Waziri Mkuu Narendra Modi kwa kuzembea katika kudhibiti machafuko ya kibaguzi ya mwaka 2002 eneo la Gujarat alipokuwa mkuu w ajimbo hilo.

Wachunguzi hawakumkuta Modi na hatia kuhusu madai hayo na kumuondolea lawama.

Tangu wakati huo Ayyub amekuwa mchambuzi anayetoa tathmini na maoni yake katika shirika la habari la Marekani Washington Post na pia katika  vyombo vingine vya habari.

Uhuru wa habari washambuliwa India, wataalam wasema

Wiki hii, Washington Post ilichapisha taarifa inayosema kila siku, Ayyub anakabiliwa na vitisho dhidi ya maisha yake na kwamba uhuru wa habari unashambuliwa nchini India.

Waandishi wengine wa habari pia wameelezea hali ya kuongezeka kwa dhuluma dhidi yao chini ya utawala wa Modi ambaye serikali yake imeshutumiwa kwa kujaribu kunyamazisha taarifa au makala ya ukosoaji kutoka kwa waandishi habari.

Ayyub mwenye umri wa miaka 37 amejikita katika uanahabari wa upekuzi na ameandika kitabu kinachomshutumu Waziri Mkuu Narendra Modi kwa kuzembea katika kudhibiti machafuko ya kibaguzi ya mwaka 2002 eneo la Gujarat alipokuwa mkuu w ajimbo hilo.
Ayyub mwenye umri wa miaka 37 amejikita katika uanahabari wa upekuzi na ameandika kitabu kinachomshutumu Waziri Mkuu Narendra Modi kwa kuzembea katika kudhibiti machafuko ya kibaguzi ya mwaka 2002 eneo la Gujarat alipokuwa mkuu w ajimbo hilo.Picha: Adnan Abidi/REUTERS

Shirika la waandishi wa habari wasio na mipaka ambalo pia hutetea haki za wanahabari (RSF), limeiorodhesha nchi ya India katika nafasi ya 142 ulimwenguni kote miongoni katika faharasa yake kuhusu Uhuru wa Habari katika nchi mbalimbali. Shirika hilo limeeleza kuwa chini ya utawala wa Modi, shinikizo dhidi ya vyombo vya habari limeongezeka kuwataka waandishi habari kufuata amri ya serikali hiyo ya kizalendo.

”Kampeni za mashambulizi mitandaoni dhidi ya waandishi habari wanaoandaa makala yanayowakosoa wafuasi wa Hindutva (misimamo mikali ya Kihindi) ni ya kutisha. Kulingana na RSF, kampeni hizo hujumuisha pia wito wa kutaka waandishi hao wauawe.

"Kampeni hizo huwa ya vurugu haswa pale walengwa ni wanawake.”

 (AFPE)