1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo kuhusu zuio la kuvaa hijab India waongezeka

Lilian Mtono
10 Februari 2022

Mamlaka katika eneo la Kusini mwa India zimefunga shule kwa siku tatu wakati kukiwa na maandamano yanayopinga zuio la wanafunzi kuvaa hijab katika baadhi ya taasisi za elimu.

https://p.dw.com/p/46npr
Indien | Protest der Muslim Students Federation MSF gegen das jüngste Hijab-Verbot
Picha: Anushree Fadnavis/REUTERS

Shule za sekondari katika jimbo la Karnataka ziliyafunga malango yake katika siku za masomo zilizosalia kwa wiki hii wakati mzozo huo ukizidi kushika kasi.

Mji mkuu wa jimbo hilo Bangalore pia umezuia waandamanaji karibu na taasisi za elimu kwa angalau wiki mbili.

Maandamano hayo yamegeuka kuwa vurugu kufuatia uamuzi huo kwa baadhi ya vyuo kuzuia wanafunzi wa kike kuvaa hijab ama vitambaa vya kichwani wakiwa madarasani.

Kufuatia zuio hilo kulizuka makabiliano kati ya wanafunzi wa Kiislamu wanaopinga na wanaounga mkono zuio hilo tangu siku ya Jumanne huku mjadala katika eneo hilo la Kusini mwa India ukiongezeka kuhusiana na ama maafisa watekeleze hatua hiyo ama la.