1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Ujenzi wa Gaza baada ya vita kuchukua hadi miaka 80

2 Mei 2024

Umoja wa Mataifa umetoa makadirio na kusema itachukua hadi miaka 80 kuujenga upya Ukanda wa Gaza na kwamba zoezi hilo litagharimu dola bilioni 30 hadi 40.

https://p.dw.com/p/4fROw
Gaza | Moja ya maeneo ya Ukanda wa Gaza ambayo yameharibiwa kutokana na vita
Moja ya maeneo ya Ukanda wa Gaza ambayo yameharibiwa kutokana na vitaPicha: Ali Jadallah/Anadolu/picture alliance

Tathmini hiyo inayolenga kutoa makadirio ya athari za kiuchumi na kijamii, imetolewa na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).

Lakini ripoti hiyo imesema ikiwa vifaa vya ujenzi vitatolewa kwa haraka kama ilivyokuwa wakati wa mgogoro wa mwaka 2021, basi muda huo unaweza kupungua na kushuhudia ujenzi wa Gaza ukikamilika ifikapo mwaka 2040.

Soma pia:Itachukuwa miaka 16, dola bilioni 40 kuijenga tena Gaza - UM

Vita vya Israel huko Gaza ambavyo vimedumu karibu miezi saba sasa, vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 34,500 pamoja na uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu.

Takwimu za mamlaka ya Palestina zinaonyesha pia kuwa karibu nyumba 80,000 zimeharibiwa.