Umwagaji damu waendelea Syria
8 Mei 2011Matangazo
Wanaharakati nchini humo wamesema, miongoni mwa watu waliouawa ni waandamanaji wanne wa kike waliokuwa wakigombea kuachiliwa huru kwa watu waliokamatwa.
Ripoti zimesema kuwa idadi kadhaa ya vifaru na magari ya kijeshi yameingia mji huo wa kaskazini-magharibi.
Makundi ya haki za binaadamu yanasema takriban watu 26 waliuawa siku ya Ijumaa katika maandamano yaliyofanywa kote nchini kuishinikiza serikali ya mabavu ya Rais Bashar al-Assad wa Syria kuondoka madarakani.
Umoja wa Ulaya umeweka vikwazo vya silaha dhidi ya Syria na marufuku ya kusafiri dhidi ya maafisa 13 wa serikali hiyo na mali yao pia imezuiliwa. Marekani nayo imetishia kuchukua hatua mpya dhidi ya kile kilichoitwa "vitendo vya kusikitisha" vinavyofanywa na serikali ya Syria.