Umoja wa Mataifa wataka Myanmar iondolewe vikwazo | Matukio ya Kisiasa | DW | 30.04.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Umoja wa Mataifa wataka Myanmar iondolewe vikwazo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyataka mataifa ya Magharibi kulegeza zaidi vikwazo vyao dhidi ya Myanmar ikiwa njia bora ya kuunga mkono mabadiliko ya kidemokrasia katika taifa hilo la kusini mwa Asia.

Myanmar's President Thein Sein (L) and United Nations Secretary General Ban Ki-moon shake hands before their meeting at the Presidential Palace in Naypyitaw April 30, 2012. Ban met Myanmar Thein Sein on Monday to offer international help for reform in the long-isolated state and will later become the first foreign dignitary to address its fledgling parliament. REUTERS/Soe Zeya Tun (MYANMAR - Tags: POLITICS TPX IMAGES OF THE DAY PROFILE)

Katibu Mkuu Ban Ki Moon

Katibu Mkuu huyo amezungumza hayo alipolihutubia bunge la nchi hiyo leo, sehemu ya ziara yake ya siku tatu nchini Myanmar. Hotuba hiyo aliitoa baada ya mazungumzo yake na Rais Thein Sein.

Ki-moon aliliambia bunge hilo kwamba anakaribisha jitihada za jumuiya za kimatiafa huku akisema vitendo zaidi katika kufanikisha ustawi wa Myanmar vinahitajika.

Alisisitiza kwamba jamii za kimataifa zinapaswa kuondoa, kusimamisha au kulegeza vikwazo vya kibiashara pamoja na vinginevyo ili taifa hilo lisonge mbele.

Myanmar's pro-democracy leader Aung San Suu Kyi attends a ceremony at National League for Democracy party head office in Yangon April 18, 2012. NLD held the ceremony to pay obeisance to the elderly members of the party in accordance with Myanmar traditions. REUTERS/Soe Zeya Tun (MYANMAR - Tags: POLITICS SOCIETY)

Mwanaharakati Aung San Suu Kyi

Kiongozi huyo pia anatarajiwa kukutana na kiongozi wa upinzani nchini humo Aung San Suu Kyi, katika ziara yake hiyo ya kwanza kuifanya tangu taifa hilo lililokuwa likijulikana kama Burma kuhitimisha utawala wa kijeshi ambao ulidumu kwa miongo kadhaa.

Hata hivyo Suu Kyii hakuwepo bungeni wakati Ki moon akihutubia bunge kwa kuwa kiongozi huyo na wenzake kadhaa walikuwa katika mgomo wa kupinga vifungu vya katika ya nchi hiyo.

Awali katika mazungumzo yake na rais Thein Sein katibu mkuu wa umoja wa mataifa ofisi yake itasaidia taifa hilo kufanikisha sensa ya kwanza kufanyika kwa kipindi cha miaka 31.

Miongoni mwa maeneo ambayo watasaidia ni pamoja na ufundi na kuwezesha upatikanaji wa fedha. Rais Thein Sein ambae ni mkuu wa jeshi wa zamani ameonesha nia ya kufanikisha mabadiliko nchini humo tangu aingie madarakani.

Miongoni mwa mambo muhimu aliyoweza kuyafanya ni pamoja na kuruhusu chama cha siasa cha upinzani kinachoongozwa na mwanaharakati Suu Kyi pamoja na kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa.

Pamoja na mambo mengine kwa upande wake Ban Ki-moon anatarajiwa kuitaka mamlaka ya taifa hilo kuruhusu misaada ya kibinadamu ya umoja mataifa kwa maelfu ya wakimbizi waliotokana na mapigano kati ya wanajeshi na kabila dogo lililoasi katika jimbo la kaskazini ya mbali la Kachin.

Pamoja na Umoja wa Mataifa kufanikiwa kutuma ujumbe wake wa usaidizi katika eneo hilo hivi karibuni lakini bado watu wengi wameendelea kuishi katika mkwamo mkubwa huku hali hiyo ikitabiriwa uenda ikawa mbaya zaidi.

Sambamba na yanayotokea sasa Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu kabisa katika Umoja wa Ulaya Catherine Ashton nae yupo Myanmar kwa ajili ya mazungumzo na rais wa taifa hilo baada ya umoja huo kusimamisha vikwazo vyake dhidi ya taifa hilo .

Mwandishi: Sudi Mnette/ AFP
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com