1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Hochkommissarin für Menschenrechte Michelle Bachelet
Picha: Martial Trezzini/KEYSTONE/dpa/picture alliance

Ethiopia: UN yalaani mapigano kati ya Wakristo na Waislamu

Zainab Aziz Mhariri:Hawa Bihoga
7 Mei 2022

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Michelle Bachelet, ameeleza wasiwasi kutokana na mapigano makali kati ya Waislamu na Wakristo wa madhehebu ya Orthodox nchini Ethiopia.

https://p.dw.com/p/4Ay0d

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu amesema amehuzunishwa sana na ghasia hizo zilizotokea mwishoni mwa mwezi uliopita katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia, ambapo takriban watu 30 waliuawa na wengine zaidi ya 100 walijeruhiwa.

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Hakim za Binadamu Michelle Bachelet
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Hakim za Binadamu Michelle BacheletPicha: AP

Mapigano hayo yalianza katika mji wa Gondar katika jimbo la Amhara na yalihusiana na mzozo wa ardhi, lakini yalienea haraka katika mikoa mingine hadi kwenye mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Soma:Kamati ya Nobel yasema Abiy ana jukumu maalumu katika mzozo wa Tigray

Baraza la Wiislamu la Amhara limesema vurugu zilitokea wakati wa mazishi ya mzee mmoja mwislamu na kulieleza tukio hilo kama mauaji ya kukusudia yaliyofanywa wakristo wenye itikadi kali waliokuwa na silaha nzito. Makaburi ambapo shambulio hilo lilitokea yapo jirani na msikiti na kanisa na ni eneo la mzozo unaoendelea kati ya Waislamu na Wakristo wa kanisa la Orthodox, ambalo ni kubwa nchini Ethiopia.

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Michelle Bachelet katika taarifa yake ameelezea masikitiko yake kutokana na misikiti miwili kuchomwa na mingine miwili iliyoharibiwa kidogo katika mji wa Gondar. Amesema katika mashambulizi ya kulipiza kisasi wanaume wawili wakristo wa kanisa la Orthodox waliyteketezwa hadi kufa na mwingine aliuawa kwa kukatwakatwa na makanisa matano yalichomwa moto katika eneo la kusini magharibi mwa Ethiopia.

Polisi wamewakamata na kuwazuia watu 578 katika takriban miji minne kuhusiana na mapigano hayo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy AhmedPicha: Tiksa Negeri/REUTERS

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Michelle Bachelet ameitaka mamlaka nchini Ethiopia kufanya uchunguzi na kisha kuwachukulia hatua za kisheria wote waliochochea pia wito wa kuchukuliwa hatua zaidi za kuzipatanisha jamii nchini Ethiopia, Ili kuzuia vurugu za kidini.

Chanzo: AFP