Umoja wa Mataifa wailaumu DRC kubana uhuru wa maoni | Matukio ya Afrika | DW | 02.12.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Umoja wa Mataifa wailaumu DRC kubana uhuru wa maoni

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya uhuru wa kutoa maoni ameishutumu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kukiuka sheria ya kimataifa juu ya haki za binadamu.

Msimamo huu unakuja huku serikali ya Rais Joseph Kabila ikichukuwa hatua yake ya kuyazima matangazo ya radio pamoja na kuwakamata waandishi habari nchini humo.

Mtaalamu huyo, David Kaye, anasema sheria iliyopitishwa Novemba 12 ya kuyazuia mashirika ya habari ya kimataifa kuendesha kazi zao nchini Kongo hadi pale yatakaposaini makubaliano na vyombo vya habari vya ndani au kuanzisha matawi yao yatakayosimamiwa na Wakongomani ni uvunjaji wa sheria za kimataifa.

Mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kupitia taarifa yake kwamba kuzimwa kwa sauti za kuikosoa serikali kwa kupitia njia ya kuwakamata, kuwadhibiti na kupitia njia nyingine za zinazotumiwa na serikali kudhibiti ni mambo yanayotishia usalama wa nchi hiyo.