1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya kimataifa waijadili Kabul

2 Mei 2023

Wajumbe kutoka nchi kadhaa pamoja na taasisi za Kimataifa jana Jumatatu walikuwa na mkutano mjini Doha, Qatar kuhusu Afghanistan uliojikita kwenye suala la haki za wanawake chini ya utawala wa Taliban.

https://p.dw.com/p/4QnPk
Katar Doha Taliban
Picha: REUTERS

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric aliweka wazi kwamba suala la kutambuliwa utawala wa Taliban haliko kwenye mjadala.

Mkuu wa ofisi ya Taliban ya masuala ya kisiasa mjini Doha, Suhail Shaheen ameonya kwamba kutohusishwa kwa serikali ya Taliban katika mkutano huo ni hatua isiyokuwa na tija.

Katika mkutano huo wa faragha wa siku mbili mjini  Doha Watawala wa Afghanistan hawakushiriki.

Wajumbe kutoka Marekani, Urusi, China na nchi nyingine 20 pamoja na taasisi nyingine ikiwemo wafadhili wakubwa wa shughuli za msaada kutoka Umoja wa Ulaya na majirani wa Afghanistan, kama Pakistan waliungana na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye mkutano huo.

Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja huo Stephane Dujarric, Katibu mkuu, anataka maelewano ya pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kuhusu namna ya kuwashirikisha Taliban katika masuala muhimu kama haki za binadamu.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW