Umoja wa Afrika wakutana kuzungumzia Kongo | Matukio ya Afrika | DW | 27.12.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Umoja wa Afrika wakutana kuzungumzia Kongo

Viongozi wa Umoja wa Afrika wanakutana kuzungumzia pendekezo la uwezekano wa kupeleka kikosi vya kulinda amani katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako waasi wa M23 wanapambana na serikali.

Wapiganaji wa M23 wakiondoka Goma mwezi Disemba huku polisi wakisimama mbele yao.

Wapiganaji wa M23 wakiondoka Goma mwezi Disemba huku polisi wakisimama mbele yao.

Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika mjini Addis-Ababa, Ethiopia, ukiwa unahudhuriwa na viongozi wa Kanda ya Maziwa Makuu, maafisa wa Umoja wa Ulaya na wawakilishi kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Ghasia zilizuka eneo hilo la mashariki mwa Kongo takriban mwezi mmoja uliopita baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma.

Mapema mwezi huu Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ilisema iko tayari kupeleka kikosi cha kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Josephat Charo